Jumapili 26 Oktoba 2025 - 19:16
Umoja wa Maulamaa na Wanafikra katika Ulimwengu wa Kiislamu ni Sharti Lisilopingika kwa Ajili ya Kuhuisha Utamaduni wa Kiislamu

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Muhammad Saeed Wa’idhy, mmoja wa wajumbe wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom, katika mkutano wa maulamaa na wanafikra kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Kiislamu na Kiufundi cha Gaziantep nchini Uturuki, alisisitiza umuhimu wa mshikamano na umoja kati ya viongozi wa kidini na wanafikra katika ulimwengu wa Kiislamu kwa ajili ya kuunda tamaduni mpya ya Kiislamu na kuimarisha umma mmoja.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Wa’idhy, ambaye pia ni mhadhiri katika Hawza ya Qom, katika dhifa ya jioni iliyoandaliwa na uongozi wa Chuo Kikuu cha Kiislamu na Kiufundi cha Gaziantep, iliyohudhuriwa na kundi la wasomi, maulamaa na wanafikra kutoka nchi za Kiislamu, alielezea changamoto na vikwazo vinavyokwamisha kuufanya wa Kiislamu kuwa pamoja.

Katika hotuba yake, alisisitiza umuhimu wa mshikamano wa umma wa Kiislamu na akasema: "Ubaguzi wa kimadhehebu na kuangazia tofauti ndogo ndogo baina ya madhehebu ni miongoni mwa vikwazo vikuu vinavyokwamisha kuundwa kwa umma mmoja na tamaduni mpya ya Kiislamu."

Mhadhiri huyo wa Hawza ya Qom alibainisha kuwa: "Umma wa Kiislamu na madhehebu mbalimbali vinaungana katika mambo mengi kifikra, utamaduni na itikadi, ambavyo vinaweza kuwa msingi wa umoja wa kweli na sababu ya kuleta ukaribu zaidi baina ya mataifa na wanafikra katika ulimwengu wa Kiislamu."

Katika hitimisho la hotuba yake, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Wa’idhy alisisitiza kwamba: "Kuimarisha mshikamano na ushirikiano wa kifikra kati ya maulamaa na wasomi ni jambo la lazima ili kuvuka changamoto zilizopo na kutimiza lengo kuu la kuanzisha tamaduni mpya ya Kiislamu."

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha